Watu
watatu wamefanya mauaji ya kutisha, wawili wamechinja wake zao, huku
mmoja akiacha ujumbe wa kumtaka mama yake mzazi amtunzuie watoto na
mwingine amemuua mama yake.
Katika
tukio la Dodoma, Samson Joramu(44), mkazi wa Chololo, Kata ya Kikombo,
alimchinja mke wake, Rehema Joram (43) kabla ya kujiua kwa kunyonga
katika shamba lake.
Watu walioshuhudia walisema, Joramu baada ya kumuua mkewe alijinyonga na aliandika ujumbe uliokutwa mfukoni kwake, ukisomeka: “Mama tunza wanangu, mimi nimekufa.” Kadhalika aliandika orodha ya watu anaowadai.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Lazaro Mambosasa akizungumzia tukio hilo alisema kuwa: “Ni
kweli taarifa za vifo kutoka Kikombo ninazo, yule mmoja alimuua mama
yake kwa kumkatakata sehemu mbalimbali za mwili jana (juzi), na huyu
mwingine alimuua mke wake asubuhi ya leo (jana) kisha naye akajinyonga,”
alisema.
Katika
tukio jingine, Amos Kalenda, mkazi wa Kikombo, Dodoma anadaiwa kumuua
mama yake mzazi, Joyce Kalenda kwa kumchinja. Chanzo cha mauaji hayo
kinadaiwa ni mama huyo kumnyima chakula.
Mkoani
Mara katika Wilaya ya Tarime, Wambura Mariba (50) mkazi wa Matongo,
Nyamongo, Tarime, anadaiwa kumuua kwa kumchinja mkewe, Maria Wambura(40)
kwa madai anamroga.
Kamanda wa Polisi Tarime/Rorya, Andrew Satta alisema tukio hilo lilitokea Juni 8 saa tisa alasiri.
Satta alisema baada ya mtuhumiwa kutekeleza mauaji hayo, alichoma moto nyumba zao mbili, zilizokuwa zimeezekwa kwa nyasi.
“Baada ya tukio hilo kutokea, wananchi walijichukulia sheria mkononi na kumjeruhi mtuhumiwa kichwani na kitu chenye ncha kali,”alisema Satta.
Wakizungumzia
tukio hilo ndugu wa marehemu, Samwel Wambura alisema tukio la mwanamke
huyo kuuawa, lilitekelezwa mbele ya watoto wake wakati akiwaandalia
chakula.
“Alipomaliza
kumuua, alianza kuandaa moto achome nyumba ili mwili wa mkewe uungulie
ndani, majirani waliwahi kuuchukua mwili, lakini alianza kuwafukuza huku
akiwa ameshika panga,” alisema na kuongeza: “Wananchi baada ya kuona tukio hilo walipiga simu kituo cha polisi ambao walifika na kumkamata mtuhumiwa.”
Mganga
Mfawidhi wa Kituo cha Afya Nyangoto, Kagumiwa Kaijage alisema, alipokea
mwili wa marehemu ukiwa umekatwa shingoni na mtuhumiwa amelazwa
hospitali hapo akiwa na majeraha sehemu mbalimbali mwilini.
0 comments:
Post a Comment