Aliyekuwa katibu mkuu wa UEFA, Gianni alipata kura 88, ikiwa ni kura tatu zaidi ya mpinzani wake wa karibu Sheikh Salman hivyo kuamriwa uchaguzi uingie katika hatua ya pili kwa mara ya kwanza tangu ilipotokea hivyo mwaka 1974.
Wajumbe kutoka mataifa 207 yanayotambuliwa na Fifa duniani wameshiriki uchaguzi huo mjini Zurich kuamua mrithi wa Sepp Blatter.
Kabla ya upigaji kura kuanza, mageuzi kadha yalipitishwa, lengo likiwa kufanya Fifa kuwa na uwazi na uwajibikaji zaidi.
Kufuatia mabadiliko hayo, mishahara yote ya maafisa wa Fifa inafaa kuwekwa wazi siku za usoni.Kutakuwa pia na kipimo kwenye muhula wa urais.
Baraza jipya pia litaundwa kuchukua nafasi ya kamati kuu tendaji, ambalo litakuwa na mwakilishi mwanamke kutoka kila shirikisho.
0 comments:
Post a Comment