Mbunge wa Kawe jijini Dar es Salaam, Halima James Mdee, jana amezua
mjadala bungeni baada ya kuweka wazi kuwa anakerwa na kitendo
kinachotajwa na baadhi ya Wabunge kwamba Rais hatajwi wala haguswi na
hoja.
Akichangia Bungeni jana, Mdee alidai wakati Rais Magufuli alipokuwa
waziri wa Ujenzi walipanga kukarabati barabara ya kilometa 5004 lakini
zikakarabatiwa 2700 pekee.
Wabunge wa CCM walicharuka wakimtaka Halima, kutotumia wala kumtaja Rais kwa Dhihaka kwa kuwa kanuni za Bunge haziruhusu.
“Kwa mujibu wa kanuni ya 64 fasili ya kwanza, Mbunge hatotumia kwa
dhihaka jina la Rais katika mjadala, Mbunge anayeendelea anatumia jina
la Rais kwa Dhihaka naomba aendelee bila kumtaja” Alisikika Mbunge mmoja
wa chama cha Mapinduzi.
Mbunge huyo kijana wa CHADEMA, alijibu hoja hiyo kwa kusema jukumu la Bunge ni kuirekebisha Serikali hivyo yuko sawa kumtaja.
“Nasema hivi hii biashara ya kufanya rais ni mtu ambae hashikiki wala
hatajwi wala haguswi iachwe, kwa sababu jukumu la Bunge ni kuirekebisha
na kushauri Serikali” Alisema.
0 comments:
Post a Comment