Mtumishi wenu JOSEPH LEONARD HAULE Ndiye mbunge halali wa jimbo la MIKUMI 2015-2020.
UKWELI UNA TABIA YA KUSHINDA SIKU ZOTE!!! Ndugu zangu wote wapenda HAKI na UKWELI napenda kuwatangazia rasmi kuwa ile kesi ya kupinga matokeo yangu ya ubunge wa jimbo la Mikumi IMEFUTWA RASMI baada ya mlalamikaji JONAS E. NKYA kushindwa kulipa gharama za dhamana ya kesi sh milioni 15 ndani ya siku 14 kama alivyotakiwa na mahakama kuu.
Hivyo basi mheshimiwa JAJI KITUTSI ameifutilia mbali na kumtaka mlalamikaji JONAS alipe na gharama zote zilizotokana na shauri hilo, Heshima kubwa sana kwa wakili Msomi sana TUNDU LISSU na Timu yake yote!!!
NB>Mtumishi wenu JOSEPH LEONARD HAULE Ndie mbunge halali wa jimbo la MIKUMI 2015-2020, Nawaomba sana ushirikiano zaidi na zaidi ili tuweze kuijenga MIKUMI yetu tunayoitaka yenye maendeleo kwa watu wote! ASANTENI SANA... MUNGU AWABARIKI SANA! !!
0 comments:
Post a Comment