Waendesha mashtaka nchini Brazil
wamependekeza kwamba nyota wa timu ya Barcelona Neymar ashtakiwe na
mashtaka matatu ya ufisadi kuhusu kesi ya kodi wakati wa uhamisho wake
hadi Barcelona.
Inadaiwa kwamba kampuni zilibuniwa ili kutumika kwa niaba yake ili mchezaji huyo alipe kodi ya kiwango cha chini.
Maafisa nchini Brazil wanasema kuwa madai hayo dhidi ya mshambuliaji
huyo wa Barcelona yanasimamia kipindi cha miaka saba kuanzia 2006.Madai
hayo ni tofauti na yale ya kesi iliosikilizwa siku ya Jumanne nchini
Uhispania.
Neymar alihudhuria kesi yake ya madai ya ufisadi kuhusu uhamisho wake.Amekana kufanya makosa yoyote.
Waendesha mashtaka wa serikali ambao wanapendekeza kushtakiwa kwake
wanadai kwamba kampuni zilibuniwa na fedha ambazo zingelipishwa kodi
katika kiwango cha mtu binafsi zilitumwa katika kampuni hizo ili
kupunguza ada hiyo.
Ni mapema mno.
Madai hayo ya viongozi wa mashtaka yatakwenda kwa jaji ambaye ataamua
iwapo kuna kesi ya kujibu au la.kwa sasa Neymar sio mshtakiwa.
0 comments:
Post a Comment