Katibu Mkuu wa WIZARA ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto , Dk. Ulisubisya Mpoki amesema kuwa Saratani ni ugonjwa ambao
unaathiri watu wa rika na jinsia zote; watoto, watu wazima, wake kwa
waume.
Kwa upande wa wanaume,Saratani ya Ngozi ,Saratani ya Koo, Saratani ya Tezi Dume, pamoja na Saratani ya Tezi,na wanawake ni Saratani ya Shingo ya Kizazi, Saratani ya Ngozi, Saratani ya Matiti, pamoja na Saratani ya Koo.
Takwimu za Shirika la Kimataifa la Atomiki la Utafiti wa Saratani (IARC)
na Shirika la Afya Duniani (WHO) zinaelezea kwamba kila mwaka duniani
kunatokea wagonjwa wapya wa saratani wanaokadiriwa kufikia milioni 14.1,
kati ya hao, zaidi ya wagonjwa milioni 8.2 hufariki dunia kutokana na
ugonjwa wa Saratani, hii husababishwa kwa wagonjwa kuchelewa kufikishwa
kwenye vituo vya kutolea huduma za afya. Vifo vya ugonjwa wa Saratani ni
asilimia 13 ya vifo vyote vinavyotokea duniani (WHO).
Tizama video hapa chini kwenye kongamano la Saratani;
Tizama video hapa chini kwenye kongamano la Saratani;
Amesema
tatizo la Saratani limekuwa likiongezeka na kukua, kila mwaka,
Takribani wagonjwa wapya wapatao 44,000 hugundulika na saratani za aina
mbalimbali nchini, hii ni sawa asilimia 10 tu (4,400) kati ya wagonjwa
wote wanaofanikiwa kufika katika Taasisi ya Saratani Ocean Road ili
kuweza kupata tiba.
Kati ya hao wanaobahatika kufika katika Taasisi ya Saratani ya Ocean
Road (takribani asilimia 80) hufika wakiwa katika hatua za mwisho za
ugonjwa (Hatua ya 3 na ya 4), hali ambayo hupunguza uwezekano wa
wagonjwa kuweza kupona maradhi hayo.
Dk.Mpoki kwa mujibu wa taarifa kutoka Taasisi ya Saratani ya Ocean
Road hapa nchini zinaonyesha kwamba aina za Saratani zinaoongoza ni kama
ifuatavyo:
Kwa upande wa wanaume,Saratani ya Ngozi ,Saratani ya Koo, Saratani ya Tezi Dume, pamoja na Saratani ya Tezi,na wanawake ni Saratani ya Shingo ya Kizazi, Saratani ya Ngozi, Saratani ya Matiti, pamoja na Saratani ya Koo.
0 comments:
Post a Comment