Mwanasiasa mkongwe aliyekuwa waziri kwenye Serikali za Awamu Nne za
Kwanza, Stephen Wasira amesema hana uhakika kama muundo wa Serikali ya
Rais John Magufuli unapunguza matumizi ya fedha za umma.
Wasira anakuwa waziri wa tatu wa Serikali ya Awamu ya Nne kuzungumzia
sera za kubana matumizi za Rais Magufuli, baada ya Bernard Membe na Dk
Makongoro Mahanga kusema kuunganisha wizara na kubakia na idadi kubwa ya
makatibu wakuu si kubana matumizi.
Baraza ambalo Rais Magufuli alilitangaza lina mawaziri 34, ikiwa ni
pungufu ya mawaziri 20 ikilinganishwa na baraza la mwisho la Rais Jakaya
Kikwete, huku kukiwa na wizara 18, baadhi zikiwa zimebakia na makatibu
wake wakuu licha ya kuunganishwa.
Akizungumza kwenye mahojiano maalumu na Mwananchi, Wasira alisema licha
ya Rais Magufuli kupunguza idadi ya mawaziri ikilinganishwa na
mtangulizi wake, jambo hilo halimaanishi kwamba Serikali itatumia fedha
kidogo.
Wasira, ambaye alikuwa miongoni mwa wana-CCM waliojitokeza kutaka
kuteuliwa na chama hicho kuwania urais, alisema mtazamo kuhusu baraza la
mawaziri unategemea malengo ya kiongozi husika.
========================================================
========================================================
TANGAZA NASI KWA VITU VIFUATAVYO;
1. Biashara / Maduka na Bidhaa / Ofisi 2. Kuuza Nyumba / Kupangisha 3. Kuuza Magari / Pikipiki 4. Kuuza Viwanja / Mashamba 5. Matangazo Mbalimbali 6. Matangazo ya Mikutano / Sherehe 7. Matangazo Shule / Course za Masomo Mbalimbali 8. Hotel / Restaurat
Tunapokea matangazo yako sasa Tangaza na TBN_MUSSANKONINGO.BLOGSPOT.COM kukuza Bishara yako.. Wasiliana nasi Kwa simu namba 0755933877/0787260182. Au EMAIL@MUSSABAKARINKONINGO@GMAIL.COM.

0 comments:
Post a Comment