Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mh. Mama Samia Suluhu amemfuta machozi Mwanadada,Happiness
Millen Magese ambaye ni shujaa wa kipekee kutoka Afrika dhidi ya
mapambano ya ugonjwa wa Endometriosis.
Mama Samia amechukua hatua hiyo jioni ya 15 Aprili 2016 wakati wa hafla maalum ya kumkabidhi tuzo.
Katika kilio chake hicho
Millen, kimemfanya Mama Samia kumfuta machozi na kumpa kitambaa,
mwanamitindo huyo huku akimweleza kuwa, Serikali itaendelea kushirikiana
naye kwani tatizo hilo si la Millen pekee bali ni kwa wanawake wengi
hapa Tanzania.
Mama Samia alimwambia
kuwa, tatizo alilonalo la kuziba kwa mirija ya uzazi lipata ufumbuzi na
kutaka asilie kwani Serikali inania njema kwa watu wake hivyo
wataendeleza juhudi Zaidi huku akifungua milango na mwanadada huyo.
Suluhu
alisema kuwa hata yeye tatizo kama hilo lipo katika familia yake, lakini
ana amini kwa ushirikiano wa mwanamitindo huyo tatizo hilo linapewa
uzito. Alisema kuwa ni kitu kilichokuwa kikimuumiza sana kichwa, ana amini kupitia Millen hata binti yake atapata nafuu.
"Nimefurahi kukutana nawe
na Serikali haitakuangusha tutakuunga mkono katika kuhakikisha gonjwa
hili linapata ufumbuzi na kutoa elimu kwa kila mtanzania
kulitambua"alisema.
Akizungumza kwa upande
wake Magese alisema amekuwa akifanya semina mbalimbali kwa kushirikiana
na madaktari bingwa wa Hospitali ya Taifa, Muhimbili, kuwaelimisha
wanawake kuhusu endometriosis.
"Ninaamini
-Nikiokoa hata nafsi moja kuna wakati ambao inatosha kwani nafsi hiyo
yaweza kuokoa walio wengi zaidi,shabaha yake ni kuona wanawake wenye
ugonjwa huo wanapata tiba mapema ili waweze kubaki na uwezo wao wa kushika mimba na kuzaa kwa njia ya kawaida" alisema Magese.
"Mimi nilichelewa na
nimejikuta nikipoteza uwezo wa kushika mimba, kwa hiyo siwezi tena
kupata mtoto kwa njia ya kawaida, Kibaiolojia.
"Nimeshafanyiwa oparesheni
mara 13 kati ya Afrika Kusini na Marekani. Na sasa mirija yangu yote ya
uzazi imeziba, vilevile upande mmoja wa ovari haufanyi kazi".
"Naahidi kupambana na
ugonjwa huu mpaka mwisho. Pamoja na jitihada zote, lengo langu la juu ni
kuhakikisha napata uwezo wa kujenga hospitali kubwa kupitia taasisi
yangu ya Millen Magese (Millen Magese Foundation) ambayo
itajishughulisha zaidi na utoaji wa tiba ya endometriosis kwa wanawake.
Namuomba sana Mungu anisaidie."
Picha zaidi hapa chini..........
0 comments:
Post a Comment