Chukua hii..!! Suala la wachezaji kuvaa jezi namba flani mgongoni mara
nyingi huwa linaongozwa na imani au pengine mapenzi ya mchezaji mwenyewe
,ila hii hapa ni list ya wachezaji saba ambao wamewahi kufanya mambo
makubwa kwenye historia ya soka ulimwenguni,wakiwa wamevaa jezi namba 7
mgongoni.
Robert Pires alidumu kwenye kikosi cha Arsenal kwa miaka 6 pekee lakini
ilitosha kumpa heshima kwenye klabu hiyo na kuwa miongoni mwa wachezaji
wa kukumbukwa kwenye historia ya Arenal.Baada ya mafanikio makubwa
kwenye michuano ya kombe la dunia na Euro mwaka 1998 na 2000 akiwa na
timu ya taifa ya Ufaransa, Pires alijiunga na The Gunners na kukiongoza
kikosi hicho kutwaa makombe matatu ya FA na mataji mawili ya Premier
League.
Luis Figo anatajwa kama nahodha wa aina yake kuwahi kutokea kwenye timu
ya taifa ya Ureno ambaye alikuwa akivaa jezi namba 7 na kupata mafanikio
makubwa. Winga huyu aliekua na uwezo hali ya juu kipindi cha uchezaji
wake, anasifika kwa uwezo wake mkubwa wa kukimbia na mpira huku
akiwaacha mabeki ikiwa ni pamoja na kutengeneza nafasi kwa wachezaji
wenzake kufunga mabao.Licha ya kutotwaa taji lolote akiwa na timu yake
ya taifa,Luis Figo lakini anabaki kuwa miongoni wachezaji bora kuwahi
Ureno na anakumbukwa zaidi na mashabiki wa Inetr Milan na Real
Madrid,vilabu alivyowahi kuvitumikia kutokana na uwezo aliounesha kwenye
historia ya michezo aliyocheza kwenye timu hizo.
Kenny Danglish alikuwa ni miongoni mwa wachezaji muhimu ndani ya
Liverpool kwenye miaka ya 1970 na1980 na anatajwa kama wachezaji bora
kuwahi kuitumikia Liverpool.Danglish Alichukua namba 7 ambayo ilikuwa
inavaliwa na mkongwe mwingine wa Liverpool Kevin Keegan, lakini
alifanikiwa kupata mafanikio kuliko alyemtangulia kuvaa jezi hiyo.
Mashabiki wa soka nchini Uingereza walimpa jina la ‘Premier League
bad boy’,ila ukweli unabaki kuwa Eric Cantona ni miongoni mwa majina
yenye heshima kuwahi kuvaa jezi namba 7 kwenye klabu ya Manchester
United.
Licha ya kuchukiwa na baadhi ya mashabiki, Cantona alifanikiwa
kuwateka mashabiki wengi wa United kutokana na uwezo alichokuwa
anakionesha uwanjani. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa alidumu
United kwa miaka 5 lakini aliweza kufunga magoli 80 na kushinda mataji
kibao ikiwemo ya mataji matatu (treble) mnamo mwaka 1999.
Garrincha ni jina maarufu kwenye historia ya soka la Brazil, anasimama
kama mchezaji bora kuwahi kutokea amabaye alikuwa akivaa jezi namba 7.
Akiwa amekiongoza kikosi cha Brazil kutwaa kombe la dunia mwaka 1972
bila ya Pele. Legend huyo wa Brazil alichaguliwa kwenye kikosi bira
cha karne ya 20 na timu ya FIFA ya wachezaji bora wa muda wote kwenye
kombe la dunia.
Star huyu anaeichezea klabu ya Real Madrid anafunga list hii ya
wachezaji waliowahi kupata mafanikio wakiwa ndani ya jezi namba 7 huku
akiwa bado na muda wa kuendelea kufanya makubwa zaidi.Ronaldo alianza
kupata mafanikio kwenye klabu ya Manchester United ambapo alionesha
uwezo wa hali ya juu kabla ya kuhamia Hispania mwaka 2009 na ameendelea
rekodi ya kufunga magoli ambayo itawachukua muda mrefu ma-striker
wengine kuivunja rekodi yake.
Credit : Shafii Dauda.
0 comments:
Post a Comment