Limbo lya Mfipa ” ni jina la kabila la Warungu. Kwa tafsiri ya moja
kwa moja kwa lugha ya Kiswahili ni Ziwa Tanganyika.
Warungu Ziwa
Tanganyika wanaliita “Liemba lya Mfipa”. Warungu wanapatikana katika
vijiji vilivyopo katika mwambao mwa Ziwa Tanganyika kata ya Kasanga
wilayani Kalambo na ni miongoni mwa makabila katika mkoa wa Rukwa.
Kabila kubwa mkoani humo ni Wafipa.
Jina hilo la Mv Liemba ni la meli ya kivita ya Ujerumani ambayo
ilinunuliwa baada ya kutekwa vitani na Uingereza. Ilinunuliwa kwa Sh
60,000 tu baada ya nchi ya Ujerumani kushindwa katika Vita Kuu ya Kwanza
ya Dunia.
Meli hiyo imetajwa kwenye kitabu cha kumbukumbu za dunia Guiness
World Book of Records kama ndio meli kongwe zaidi ulimwenguni ambayo
bado inaendelea kutoa huduma ya kubeba abiria na mizigo. Kwa sasa ina
umri wa zaidi ya miaka 113 (1913 -2016) na bado inaendelea kutoa huduma.
Mv Liemba inaendelea kutoka huduma katika Ziwa Tanganyika na ndio
meli kubwa kuliko zote inayohudumu kubeba abiria ziwani humo. Ziwa
Tanganyika lina kina na maji chenye umbali wa kilomita moja na nusu .
Inafanya safari zake kutoka bandari ya Kigoma (Tanzania), Kalemie na
Moba katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) mpaka bandari
ya Mpulungu nchini Zambia kupitia bandari ndogo ya Kasanga wilayani
Kalambo katika mkoa wa Rukwa .
0 comments:
Post a Comment