Manchester City imeanza kwa sare ya
0-0 kwenye uwanja wake wa Etihad dhidi ya Real Madrid katika mchezo wa kwanza
wa nusu fainali ya Champions League. Hiyo inamaanisha kuwa katika mchezo wa
marudiano wiki ijayo, miamba hiyo ya England itahitaji sare yoyote ya magoli
ili kutinga fainali kwa faida ya goli la ugenini.
Real Madrid wana mlima mrefu wa
kupanda nyumbani kwani ni lazima washinde mchezo huo, vinginevyo sare ya 0-0
italazimisha mshindi kupatikana kwa hatua ya matuta.
Hata hivyo Real Madrid wanaweza wakawa
na faida ya uwepo wa Cristiano Ronaldo ambaye ameukosa mchezo wa kwanza baada
ya kocha wake Zinedine Zidane kuamua kuendelea kumlinda kufuatia maumivu ya
msuli aliyoyapata tangu wiki iliyopita.
Awali Zidane alisema Ronaldo yuko
fiti lakini mwisho wa siku kocha huyo hakutaka kucheza kamari juu ya afya ya
mchezaji huyo tegemeo.
0 comments:
Post a Comment