Malalamiko
ya siku nyingi ya wasanii wa kazi za tasnia ya muziki na filamu kuibiwa
au kutumika isivyo kwa kazi zao na wao kutopata chochote kwenye kazi
hizo yamesikiwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania ‘TRA‘
ambapo walianza kulifanyia kazi suala hilo kwa kufanya msako ili kubaini
watu wanaoendesha biashara ya kuuza kanda za muziki na filamu bila
kufuata utaratibu wa sheria.
April 19 2016 Mamlaka ya Mapato Tanzania ‘TRA‘ imetoa taarifa kwamba zoezi la msako lilipelekea kukamatwa kwa jumla ya CDs na DVDs 656,579 zenye thamani inayokadiriwa kufikia bilioni 1.3. Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi wa elimu kwa walipakodi , Richard Kayombo amesema ……….
>>>’katika
zoezi hilo tulikamata wanaoshiriki kuuza kazi hizi kinyume cha
taratibu, tulikamata mitambo 47 ya kudurufu CDs na DVDs pamoja na
computer nne ambazo zinatumika katika ufanyaji wa kazi hiyo’:-Richard Kayombo
>>>‘Taarifa
za kiinteligesia zinaonyesha kuwa bado kuna CD na DVD nyingi zimefichwa
na baadhi ya wafanyabiashara wasio waaminifu kwa hiyo zoezi hili ni
endelevu na tutawafikia na kuwachukulia hatua za kisheria’:-Richard Kayomb.
0 comments:
Post a Comment