1. UN: Marekani na Urusi ziokoe amani Syria
Mjumbe maalum wa Syria, Staffan De
Mistura, ameziomba nchi mbili, Marekani na Urusi, kuzindua mikakati ya
haraka ya kiwango cha juu, yenye nia ya kuokoa mazungumzo ya amani
nchini Syria.
Baada ya kufahamisha baraza la usalama la Umoja wa
mataifa, De Mistura amesema kuwa mpango wa kukomesha mapigano nchini
humo, unayumbayumba na huenda ukasambaratika wakati wowote.
2. Watu 16 wauawa shambulio la Marekani Aleppo.
Ripoti kutoka mji wa Aleppo nchini Syria, zinasema kwamba yamkini raia
16 wameuwawa katika shambulio la angani lililolenga hospitali moja na
majumba yaliyokuwa karibu. Shambulio hilo lilitekelezwa na majeshi ya
serikali. Watoto ni miongoni mwa waliouwawa.
3. Cruz ateua mgombea mwenza.
Seneta wa Texas Ted Cruz, ambaye anatafuta nafasi ya kuteuliwa kukiwakilisha chama cha Republican kama Rais wake, katika uchaguzi mkuu wa Urais nchini Marekani amemtaja Carly Fiorina, afisa mkuu wa kampuni moja ya teknolojia kama mgombea mwenza.Bi Fiorina alikuwa mwaniaji kiti cha urais kabla ya kujiondoa katika kinyanganyiro hicho, mwezi Februari.
4. Trump akosoa sera za Obama.
Anayeongoza katika kinyang'anyiro cha kutaka kuteuliwa kugombea urais
kupitia chama cha Republikan nchini Marekani, Donald Trump, ametoa
hotuba yake ya kwanza inayohusu sera za mambo ya nje, ambapo
ameishambulia vikali sera hiyo chini ya utawala wa Rais Barack Obama.
5. Waokoaji watafuta manusura Guatemala.
Mamia ya waokoaji katika mji mkuu wa Guatemala, wanaendelea na msako
wao kuwatafuta manusura waliofunikwa na taka, baada ya jaa la taka
kuporomoka kutokana na mvua kubwa iliyonyesha.
Maiti nne zimeopolewa huku watu kadhaa wakinusuriwa, wakiwa hai. Wengi wao bado hawajulikani waliko.
6. Faida ya Facebook yaongezeka pakubwa
Na Kampuni ya mtandao wa kijamii ya Facebook imetangaza faida yake
imeongezeka mara tatu katika kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka
ikilinganishwa na kipindi sawa mwaka jana.
Kiwango hicho cha faida
kilifikia dola bilioni 1 nukta tano. Wachanganuzi wanasema kuwa hiyo ni
baada ya kuongezeka kwa mapato yatokanayo na matangazo katika simu
tamba za smartphones.
7. Maandalizi ya kuunda serikali yaendelea Sudan Kusini.
Maandalizi yanaendelea nchini Sudan Kusini ya kuunda serikali ya
umoja wa kitaifa, baada ya kurejea kwa kiongozi wa upinzani Dkt Riek
Machar mjini Juba Jumanne ya wiki hii.
Aliapishwa kama makamu wa
Rais kama sehemu ya muafaka wa amani wenye nia ya kukomesha mapigano ya
kikabila ya muda mrefu, ambapo makumi kwa maelfu ya watu wameuwawa.
chanzo;bbc.
chanzo;bbc.
0 comments:
Post a Comment