Kocha wa timu ya
Taifa ya Rwanda, Johnny McKinstry amedai kuwa klabu pambano la Azam na
Esperance ya Tunisia bado gumu sana kwa kuzingatia uzoefu wa Esperance katika
michuano ya Afrika.
Hata hivyo kocha
huyo kijana, ameongeza kuwa Azam wanaweza kuitupa nje ya mashindano Esperance
endapo watafanikiwa kupata bao la ugenini.
“Esperance ni
wazoefu katika ngazi hii. Pambano bado ni gumu sana hasa baada ya matokeo ya
2-1 hapa Tanzania. Lakini Azam wanaweza kwenda kujaribu na kumaliza kazi
waliyoianza Nyumbani. Si jambo jepesi” McKinstry aliiambia Soka360 katika
mahojiano na mtandao huu.
“Nadhani kama
wanaweza kwenda na kupata bao la ugenini , nafikiri wanaweza kufuzu. Nadhani
kwenda Tunisia na kujaribu kutafuta sare ya bila kufungana ni hatari sana” Kama wanaweza
kupata bao la ugenini watakuwa na nafasi kubwa mno ya kufuzu, siioni Azam
wakiruhusu kufungwa mabao mawili au matatu.
Azam itakabiliana na Esperance katika mchezo wa marudiano Aprili 19, jijini Tunis katika pambano la marudiano linalotarajiwa kuchezeshwa na waamuzi wa Morocco kuanzia majira ya kumi na moja na nusu kwa saa za Afrika Mashariki.
0 comments:
Post a Comment