Jino kubwa la nyangumi limepatikana
ufukweni Australia, na kuwa thibitisho la kwanza kwamba nyangumi wakubwa
hatari sana waliishi mbali na Amerika.
Mkusanyaji wa visukuku
Murray Orr alipata jino hilo lenye urefu wa sentimeta 30 (inchi 12)
ufukweni Beaumaris Bay karibu na mji wa Melbourne mwezi Februari.
Alilikabidhi kwa makumbusho ya Victoria, ambayo yalianza kulionesha kwa umma Alhamisi.
Inakadiriwa
kwamba nyangumi mwenye jino hilo aliishi zaidi ya miaka milioni tano
iliyopita. Alitoka kwa aina ya nyangumi ambao siku hizi hawapatikani
duniani.
Nyangumi hao wanaaminika kuwa watangulizi wa nyangumi wakubwa wa sasa wajulikanao kwa Kiingereza kama "sperm whales".
Makavazi hiyo imesema nyangumi mwenye jino hilo huenda alikuwa na urefu wa mita 18 na uzani wa tani 40.
0 comments:
Post a Comment