728x90 AdSpace

  • Latest News

    Sunday, April 24, 2016

    MAHAKAMA YA RUSHWA KUANZA KUFANYA KAZI JULAI, ITAANZA NA KESI 10.

    Mahakama ya Rushwa, ambayo iliahidiwa na Rais John Magufuli wakati wa Uchaguzi Mkuu uliopita, itaanza kufanya kazi Julai kwa kushughulikia kesi kumi ambazo uchunguzi wake umekamilika Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alisema hayo wakati akiwasilisha hotuba Makadirio na Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu bungeni Ijumahii.

    “Napenda kulitaarifu Bunge lako kwamba, Serikali imeanzisha Divisheni ya Rushwa na Ufisadi ya Mahakama Kuu itakayoanza kufanya kazi Julai mwaka 2016,” alisema Majaliwa.

    Majaliwa alisema katika mwaka wa fedha wa 2016/17 Serikali itaendelea kuchunguza tuhuma 3,444 zilizopo na mpya zitakazojitokeza na kukamilisha uchunguzi wa tuhuma 10 za rushwa kubwa.

    Waziri Mkuu Majaliwa alisema kuanzishwa kwa mahakama hiyo ni ahadi iliyotolewa na Magufuli wakati akilihutubia Bunge Novemba mwaka jana baada ya kuapishwa.

    Januari mwaka huu, Rais Magufuli alimtaka Jaji Mkuu, Othman Chande kutosubiri Bunge kupitisha Sheria ya uanzishwaji wa mahakama ya mafisadi na badala yake waanze maandalizi ya kuiendesha mahakama hiyo.

    Alisema kucheleweshwa kuanzishwa kwa mahakama hiyo kutatoa mwanya na mafisadi kuendeleza kuinyonya nchi na kuifanya kuendelea kuwa masikini wakati ina rasilimali za kutosha ambazo zinaweza kuiendesha nchi bila kutegemea wafadhili.

    Chanzo;mwananchi.
     
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: MAHAKAMA YA RUSHWA KUANZA KUFANYA KAZI JULAI, ITAANZA NA KESI 10. Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top