TAARIFA KWA
VYOMBO VYA HABARI
Taasisi ya
Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Mwanza, tarehe 21/04/2016 imemfikisha
mahakamani Afisa Mtendaji wa kata ya Mwakilyambiti wilaya ya Kwimba BW.
BONAVENTURA LUPILYA MAKUNGU(46) kwa kosa la kuomba hongo ya shilingi laki tatu
(300,000/=) na kufanikiwa kupokea
shilingi (190,000/=) kutoka kwa JOHN MASHOMALI LUKUNGU(45).
Afisa mtendaji
huyo aliomba pesa hiyo ili aweze kumpatia dhamana ndugu wa bwana JOHN MASHOMALI
LUKUNGU(45), Bi LUCIA SOBOLA JANELA
ambaye yeye kama mlezi alikamatwa kwa kosa la utoro wa mwanafunzi LUCIA MABULA JOHN.
Mtuhumiwa BW.
BONAVENTURA LUPILYA MAKUNGU alitenda kosa hilo la kuomba na kupokea hongo mnamo
tarehe 26/02/2016 ambapo ni kinyume na kifungu cha 15(1a) cha sheria ya Kuzuia
na Kupambana na Rushwa Namba 11/2007.
Mashtaka
hayo yamefunguliwa katika Mahakama ya Wilaya ya Kwimba na Mwendesha Mashitaka
wa TAKUKURU Bw. JOVINE MAJURA ambapo
yamesajiliwa kwa shauri la jinai namba 39/2016 na liko mbele ya Mheshimiwa Hakimu BONAVENTURA
LEMA.
Akisomewa
shauri hilo mbele ya Hakimu, Mtuhumiwa BW.
BONAVENTURA LUPILYA MAKUNGU(46) alikana shtaka hilo na yuko nje kwa
dhamana hadi shauri hilo litakapotajwa
tena tarehe 24 Mei, 2016.
Wakati
huohuo TAKUKURU Mkoa wa Mwanza pia inatarajia kumfikisha mahakamani Afisa
Afya na Mazingira Bw. SOSPETER JACOB
SELEWA (29) wa kata ya Buswelu iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela, kwa
kosa la kuomba rushwa ya shilingi Laki 100,000/= kutoka kwa Bi. LYDIA JULIUS
TAMBILIJA ambaye ni mmiliki wa kituo cha kulelea watoto kinachofahamika kwa
jina la JITAMBUE.
Afisa Afya
huyo aliomba pesa hiyo ili aweze
kufungua kituo hicho cha kulelea watoto
ambacho awali alikifunga kwa vile kituo hicho hakikuwa na baadhi ya sifa
zinazostahili.
|
Imetolewa Tarehe 22/042016
na ERNEST MAKALE, Mkuu wa TAKUKURU(M)
0 comments:
Post a Comment