Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye
anatarajia kuzindua siku ya madansa duniani itakayoadhimishwa kwenye
viwanja vya TCC Club Chang’ombe, Dar es Salaam leo.
Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Tanzania Disc Association
(TMDA), Asanterabbi Mtaki, inaeleza kwamba kwa mara ya kwanza madansa
nchini wataungana na madansa wa mataifa mengine duniani kuadhimisha siku
hiyo inayoadhimishwa kila Aprili 29 ya kila mwaka.
“Lengo la maadhimisho hayo hapa nchini ni kuhamasisha madansa
kushiriki, kujitolea kufanya shughuli za kijamii kivitendo na kuongeza
uelewa ili wajitambue kuwa ni sehemu ya ajira ya kujipatia kipato,”
alieleza Mtaki.
Alisema baadhi ya madansa waliojitokeza kushiriki katika maadhimisho
hayo ni Bombes group, Wakali Dancer, Athuman digadiga bingwa wa
break-dance na funky Taifa pamoja na madj mbalimbali akiwemo Dj
Seckklito, Dj john Peter Pantalakis, Dj disko na Dj Mafuvu.
0 comments:
Post a Comment