Chama cha Waandishi wa Habari wa Kupiga Vita Matumizi ya
Dawa za Kulevya na Uhalifu Tanzania (OJADACT), Tunalaani vikali kuzuiwa kwa
Waandishi kuingia Bungeni kwa lengo la kufanya coverage (kuandaa habari) ya vikao vya Bunge la
kujadili mpango wa maendeleo ya miaka mitano na bajeti ya serikali.
OJADACT, hatukubaliani na utaratibu wa sasa wa kutumia idara
ya habari na maelezo ya Bunge, kuwa ndio wenye jukumu la kukusanya taarifa na
kuzigawa kwa waandishi.
Ni ukweli usiopingika kuwa, maamuzi hayo yana athari
zifuatazo.
Kuminya uhuru wa haki ya kupata taarifa kwa wananchi km
ilivyoainishwa kwenye katiba ya Jamhuri ya Muungano.wa.Tanzania ibara ya 18.
Kuminya uhuru wa vyombo vya habari, ambao umekuwa ukikosa
haki ya msingi iliyokosekana kwenye
Katiba.
MSIMAMO WETU.
Kwa kuwa Bunge
halioni umuhimu wa waandishi Bingeni basi tunaviomba vyombo vyote vya
habari vya binafsi kuwatoa waandishi wao bungeni.
Tunaviomba vyombo vyote vya habari vya binafsi kususia
kuandika habari za bunge hadi hapo litakapotengua utaratibu huo.
Waziri mwenye dhamana ya habari afute kauli yake ya kejeli
kuwa wanaopinga utaratibu huo eti waende Mahakamani.
Ahsanteni sana wanahabari kwa kuitikia wito wetu.
Edwin Soko
Mwenyekiti
April 24,2016
Mwanza.
Chanzo;Binagimediagroup.
Chanzo;Binagimediagroup.
0 comments:
Post a Comment