Rais Magufuli amemsimamisha kazi
mchana huu Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam Wilson Kabwe kutokana na
ufisadi wa kutisha katika utekelezwaji wa mikataba mitatu, inayohusu
maeneo ya ukusanyaji mapato ya Stendi Kuu ya Mabasi Yaendayo Mikoani ya
Ubungo na kodi ya uegeshaji magari katikati ya mji na kuisababishia
serikali hasara ya bilioni 3.
Rais
Magufuli amechukua uamuzi huo mchana huu wakati wa uzinduzi wa daraja
la Kigamboni, ambapo kabla ya Rais kuhutubia, Mkuu wa Mkoa wa Dar es
Salaam Paul Makonda alitoa Hotuba fupi ya maswala kadhaa ya Mkoa wa Dar
es Salaam ikiwemo ripoti ya tume aliyounda kuchunguza utekelezwaji
wa mikataba hiyo.
Akieleza
zaidi, Makonda amesema, Kamati aliyounda ilibaini kuwa pale ubungo
kunatumika sheria ndogo mbili za ukusanyaji mapato moja ya mwaka 2004 na
nyingine ya mwaka 2009 ambazo zote zilisainiwa na Wilson Kabwe.
Amesema
kuwa Sheria ya Mwaka 2004 ya ukusanyaji mapato, inaonesha kuwa kila
basi linaloingia Ubungo linatakiwa kutozwa Sh 4,000, hivyo makusanyo
halisi kwa mwezi ni Sh milioni 42 kutokana na mabasi 350 yanayoegeshwa
kituoni hapo na Sheria ya Mwaka 2009 ya ukusanyaji mapato,
inaonesha kuwa kila basi linaloingia Ubungo linatakiwa kutozwa Sh
8,000, hivyo makusanyo halisi kwa mwezi ni Sh milioni 82 kwa mwezi
Makonda amesema kwamba, Kabwe alisaini mikataba miwili, wa 2004 na wa mwaka 2009 ambapo ule wa mwaka 2004 ulipelekwa jiji na ule wa 2009 ukapelekwa kwa mzabuni, hivyo jiji wanajua kuwa basi linatozwa sh. 4000 kwa siku wakati mzabuni anatozwa 8000 kwa siku
Kutokana
na maelezo hayo, Mheshimiwa Rais ametangaza kumsimamisha kazi bwana
Kabwe ambaye ni Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam na ameagiza
vyombo vya dola vianze uchunguzi mara moja ili hatua zaidi za kisheria
ziweze kuchukuliwa
0 comments:
Post a Comment