Waziri wa
Katiba na Sheria Dkt.Harrison Mwakyembe (pichani) amewataka wananchi
kutomwandikia barua za malalamiko yao, badala yake watumie kamati za
maadili za kimahakama zilizopo kila Wilaya nchini ili kupata haki zao.
Mwakyembe ametoa
kauli hiyo hii leo Jijini Mwanza, anakofanya ziara ya kikazi ili
kujionea utendaji kazi wa idara mbalimbali zikiwemo za mahakama.
"Tumeunda kamati
za maadili za mahakama hivyo pelekeni barua za malalamiko kwenye hizo
kamati ambazo mwenyekiti wake ni Mkuu wa Wilaya". Amesema Mwakyembe huku
akimpongeza Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza Baraka Konisaga
kwa kuunda kamati hiyo ambayo ndani yake pia yumo Katibu tawala Wilaya,
Jaji Mfawidhi na hakimu wa Wilaya.
Amesema kwa siku
amekuwa akipokea barua za malalamiko zaidi ya 40 kutoka kwa wananchi
nyingi zikitoka Mkoani Mwanza, hivyo wananchi watumie kamati za maadili
katika wilaya zao ili kutatua malalamiko yao ikizingatiwa kwamba kamati
hizo zinafanya kazi inavyostahili.
Na:George Binagi-GB Pazzo @BMG
0 comments:
Post a Comment