BEKI wa kati wa Paris Saint-Germain,
Thiago Emiliano da Silva, maarufu kama Thiago Silva, amemtahadharisha Zlatan
Ibrahimovic kwamba kuhamia katika Premier League ni ‘kujishusha’.
Silva alisema kuwa hakuna timu England
unayoweza kuilinganisha na PSG, ambayo tayari imefanikiwa kushinda taji lake la
nne mfululizo la Ligue 1.
"Ni rafiki yangu mzuri, lakini
pia katika umri wa miaka 34 anacheza soka bora," Silva aliliambia gazeti
la Mirror. "Ni mmoja wa wabora duniani, ni wa kipekee, hakuna mchezaji
mwingine kama yeye."
"Kwa kweli nataka abaki PSG,
siwezi kufikiria tutakavyokuwa bila yeye. Najua ana ofa kutoka England – na ni
ligi kubwa – lakini sidhani kama kuna timu England ambayo ipo katika ngazi ya
PSG kwa sasa. Kwangu mimi itakuwa ni kushuka kiubora kwake."
0 comments:
Post a Comment