Wakazi wa Manipaa ya TABORA wametakiwa kuboresha usafi wa
mazingira ili kujikinga na ugonjwa hatari wa kipindupindu.
Katika mahojiano maalumu na CGFM, Afisa Afya wa Manispaa
ya TABORA,Bwana VEDASTUS CHEYO amesema baadhi ya njia za kujikinga na ugonjwa
wa kipindupindu ni kuhakikisha mazingira yanakuwa katika hali ya usafi,kujenga choo bora na kukitumia na kunawa
mikono kwa maji safi na salama kwa kutumia sabuni baada ya kutoka chooni.
Bwana CHEYO amewatahadharisha wakazi wa manispaa ya
TABORA kuwa makini na ugonjwa hatari wa kipindupindu
kwa sababu unasababisha kifo kutokana na ukosefu wa maji na madini mwilini
baada ya kuharisha na kutapika.
Ameongeza kuwa ugonjwa wa
kipindupindu pia husababisha kushuka kwa uchumi katika familia kutokana na
shughuli za uzalishaji mali kusimama ili kumhudumia mgonjwa na kushiriki katika
misiba.
Ugonjwa huo tayari umesababisha vifo kwa watu kadha
mkoani DAR ES SALAAM na sasa umeenea
hadi mikoa ya MOROGORO na PWANI.
0 comments:
Post a Comment