Wananchi katika manispaa ya TABORA wametakiwa kufuata
matumizi sahihi ya barabara ikiwa ni pamoja na sheria za barabarani ili
kuepusha ajali za barabarani.
Wito huo umetolewa na Afisa Mfawidhi wa Mmlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na
Majini -SUMATRA Bwana JOSEPH MICHAEL wakati akizungumza na na CG FM ofisini kwake kuhusu uelewa wa
wananchi juu ya elimu ya usalama barabarani.
Amewataka wananchi kufuata matumizi sahihi ya barabara na
kuacha kutumia barabara kwa mazoea.
Bwana MICHAEL pia amewahimiza wanawake wenye mazoea ya
kupanda baiskeli huku wakiwa na watoto mgongoni kuacha tabia hiyo na kusema
kuwa ni hatari kwa usalama wao hasa wanapokua barabarani.
MARIA PETER,YAHAYA SAIDI,na SAMWELI ni baadhi ya wakazi wa manispaa ya TABORA wamesema
ukosefu wa elimu na ukosefu wa miundo
mbinu ya alama za barabara ndiyo chanzo cha watu kutofuata matumizi sahihi ya barabara na
hivyo kusababisha ajali nyingi za barabarani.
Uelewa mdogo wa matumizisahihi ya barabarani kwa wananchi
umekua ukisababisha ajali za mara kwa mara katika maeneo mengi nchini.
0 comments:
Post a Comment