Bingwa wa michuano ya US Open mwaka 2015, Novak Djokovic amesema
kuna ulazima kwa mashabiki wa mchezo wa Tennis kuendelea kumuunga mkono
kutokana na mafanikio anayoendelea kuyapata.
Djokovic anayeshika namba moja kwa ubora duniani upande wa wanaume,
amezungumza maneno hayo siku moja baada ya kumshinda Roger Federer
katika mchezo wa hatua ya fainali ya michuano ya US Open ambao
ulishuhudia akishinda kwa seti tatu kwa moja ambazo ni 6-4, 5-7, 6-4 na
6-4.
Amesema anajihisi furaha kuona mashabiki wengi duniani wakiendelea
kumuunga mkono, kutokana na wingi wao unao onekana uwanjani pamoja na
katika mitandao ya kijamii kutoka katika kona zote duniani.
Kasi ya mashabiki kwa Djokovic iomeendelea kuongezeaka kutokana na
juhudi kubwa aliyoionyesha kwa mwaka huu, na kufanikiwa kutwaa mataji
matatu ya Grand Slam, kupitia michuano ya Australian Open, Wimbledon
pamoja na US Open huku akitinga katika hatua ya fainali ya michuano ya
French Open na kufungwa na Stan Wawrinka kutoka nchini Uswiz miezi
miwiwli iliyopita.
Hata hivyo hii si mara ya kwanza kwa Djokovic kutwaa mataji matatu ya
Grand Slam kwa mwaka mmoja, kwani aliwahi kufanya hivyo mwaka 2011, kwa
kujishindia mataji ya Australian Open, Wimbledon pamoja na US Open.
TAZAMA INTERVIEW YAKE BAADA YA KUTWAA TAJI LA US OPEN KATIKA KIPINDI CHA THE LATE SHOW...
TAZAMA INTERVIEW YAKE BAADA YA KUTWAA TAJI LA US OPEN KATIKA KIPINDI CHA THE LATE SHOW...
0 comments:
Post a Comment