wazazi na walezi katika manispaa ya TABORA wametakiwa
kuwapeleka watoto wao waliomaliza mitihani ya darasa la saba leo kujiunga na
mafunzo ya maandalizi kabla ya kujiunga
na elimu ya sekondari mwakani.
Akizungumza na mussankoningo.blogspot.com mara baada ya kumalizika kwa mtihani
wa darasa la saba, Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi ISIKE,Bwana CHARLES
KALELANDA amesema wazazi kwa sasa wanatakiwa kuwapeleka watoto wao kwenye
mafunzo ya maandalizi ya kujiunga na elimu ya sekondari kwa sababu mtoto akikaa muda mrefu bila kujifunza akili yake hudumaa.
Kwa upande wao wanafunzi waliomaliza mitihani yao katika
shule za msingi KITETE na ISIKE zilizopo manispaa ya TABORA wamesema matarajio
yao ni kufaulu kutokana na maandalizi
mazuri waliyokuwa nayo kabla ya kuingia katika vyumba vya mitihani yao ya
mwisho.
Hata hivyo wanafunzi
hao wamewaomba wadogo zao wote wanaobaki shuleni kusoma kwa bidii ili waweze
kufaulu katika mtihani wa mwisho na pia kuwaomba wazazi au walezi wajitahidi kuwapeleka katika mafunzo ya awali ya elimu
ya sekondari.
Mitihani ya kuhitimu elimu ya msingi ilianza
jana na kumalizika leo kote nchinI.
BOFYA PLAY KUSIKILIZA HAPA CHINI....
0 comments:
Post a Comment