Kumbukumbu maalumu kwa ajili ya kuwaenzi wahanga wa mateso
yaliyosababishwa wakati wa utawala wa hali ya hatari wa Uingereza wakati
wa vita ya Mau Mau imezinduliwa nchini Kenya.
Kumbukumbu hiyo ambayo
pia inaungwa mkono na Uingereza ilizinduliwa hapo jana na kushuhudiwa
pia na maelfu ya watu wakiwemo wale walioshiriki katika vita hiyo ya
Mau Mau.
Maelfu ya wakenya ambao kwa sasa ni watu wazima walielezea
jinsi walivyopigwa ikiwa ni pamoja na kunyanyaswa kijinsia na maafisa wa
utawala wa kiingereza wakijaribu kuzima harakati zao za ukombozi
wakati makundi kadhaa ya wakenya yalipowashambulia maafisa na wakulima
wa kiingereza waliokuwa wanashikilia maeneo makubwa ya ardhi yenye
rutuba nchini humo.
Balozi wa Uingereza nchini humo amesema kumbukumbu
hiyo inafanyika ikiwa ni sehemu ya makubaliano yaliyofikiwa nje ya
mahakama kati ya wapiganaji hao wakongwe wa vita ya Mau Mau na serikali
ya Uingereza.
0 comments:
Post a Comment