TIMES FM.
Leo nchini ufaransa kunafanyika maandamano toka kwa wakulima na wafugaji kuelekea mji mkuu wa nchi hiyo.
Makamu wa rais wa Shirikisho la Wakulima nchini Ufaransa (FNSEA),
Luc Smessaert amesema Kunatrekta zaidi ya 1500 yataelekezwa kwenda Paris
pamoja na wakulima na wafugaji zaidi ya 4000 kufanya maandamano
kushinikiza unyanyasaji wa sekta ya kilimo kwa wakulima wa nchi ya
Ufaransa.
“Bei ya Mazao imekuwa ni ya chini, pembejeo hakuna , wakulima
hatuthaminiki pengine haya maandamano yataishtua serikali kutusaidia
madai yetu haya ambayo ni kipindi kirefu tumekuwa tukiyapigia kelele”,
alisema Luc Smessaert.
Wakulima kutoka wilaya 12 watashiriki katika maandamano hayo katika
eneo la taifa. Ujumbe wa wakulima hao utapokelewa leo mchana katika mji
wa Matignon, na mwingine utakwenda Bungeni ili kufikisha malalamiko yake
kwa wabunge. Maandamano haya yenye ushawishi mkubwa yametajwa kuwa ya
kihistoria na wafugaji wengi.
0 comments:
Post a Comment