wananchi wa mtaa wa KIYUNGI,kata ya KITTE katika manispaa ya TABORA wameilalamikia Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira mjini TABORA–TUWASA- juu ya maji machafu yanayotiririka katika maeneo yao wakati Mamlaka inaposafisha matenki ya kuhifadhia maji.
Wakizungumza na CGFM wananchi hao, wamesema kitendo cha
maji hayo kutiririshwa katika maeneo yao
yanasababisha uharibifu wa barabara na kuhatarisha afya za watoto wanaochezea
kwenye maji hayo.
Pia wameitaka
TUWASA kuboresha miundo mbinu ya kupitishia maji hayo na kuweka ulinzi wa
kutosha katika maeneo yanayozunguka matenki hayo kwa ili kuepuka uharibifu wa
miundombinu ya mamlaka hiyo.
Akizungumzia malalamiko hayo, Afisa Uhusiano wa TUWASA,
Bi NAJBA BATENGA amesema mamlaka haijawahi kupokea malalamiko yoyote kutoka kwa
wananchi wa mtaa wa KIYUNGI kuhusu kero ya kutiririshwa kwa maji machafu katika
maeneo yao.
Hata hivyo TUWASA imesema itatoa ufafanuzi juu ya kero
hiyo baada ya wiki moja.
BARIKI
MMBAGA.
BOFYA PLAY KUSIKILIZA HAPA CHINI....
BOFYA PLAY KUSIKILIZA HAPA CHINI....
0 comments:
Post a Comment