MWIMBAJI
wa Tanzania mwenye makazi yake nchini Sweden, Nuru The Light ameachia
video ya wimbo wake mpya ‘L’. Nuru alifanya uzinduzi rasmi wa video hiyo
Jumamosi hii kwenye kiota kipya cha starehe, Jozi Lounge kilichopo
Msasani jijini Dar es Salaam.
Uzinduzi huo ulihudhuriwa na mastaa, marafiki zake wa karibu na mashabiki.
Video
ya wimbo huo imefanyika jijini Dar es Salaam na kuongozwa na muongozaji
na mshindi wa tuzo kibao, Adam Juma aka AJ. Mandhari ya kuvutia ya
fukwe za bahari ya Hindi yanaonekana vyema kwenye video hii na uzuri wa
Nuru unaongeza kitu cha kuvutia machoni.
Nuru
alikuwa kimya kwa takriban miaka miwili baada ya kuachia wimbo wake
‘Muhogo Andazi’ aliomshirikisha Bob Junior. Aliamua kuandika wimbo huo
wa mapenzi na kuupa jina la ‘L’ kwa kuwa herufi hiyo inawakilisha vitu
vingi chanya hasa kwenye uhusiano wa mapenzi.
‘L’
umetayarishwa nchini Sweden katika studio za Joevibes Productions na
tangu uanze kuchezwa kwenye radio mbalimbali nchini umepokelewa vizuri
na mashabiki na watangazaji wa radio hizo huku wakimtaka kueleza
alipoipata idea hiyo ya kipekee.
“L
inasimama badala ya maneno mengi chanya, inaweza kuwa Love, Light,
Love, Life na mengine mengi, vilevile nilitaka kuonesha kuwa sio lazima
wimbo uwe neno zima, ukiwa mbunifu zaidi hata herufi moja tu inaweza
kusimamia wimbo mkubwa wenye maana kama huu,” anasema.
"Pia
nilitaka kuonesha kuwa kwa msanii ni muhimu muda mwingine kupumzika
kidogo, ku-refocus, kurudi upya na kuwa na ile njaa kali ya kuandika
nyimbo bora zaidi, kusimama jukwaani na kuwa mbunifu zaidi kwa sababu
sometimes unachoka,” aliongeza.
Pamoja na Muhogo Andazi, Nuru aliwahi kutamba na nyimbo kama Walimwengu, Msela na Nisubiri Usilale.
0 comments:
Post a Comment