Mshambuliaji kutoka nchini Italia, Super Mario Barwuah Balotelli,
amedhihirisha mapenzi yake na klabu ya AC Milan licha ya kusajiliwa kwa
mkopo akitokea Liverpool, mwishoni mwa usajili wa majira ya kiangazi.
Balotelli amedhihirisha mapenzi na klabu hiyo ya mjini Milan, baada
ya kupiga picha ya kuianika hadharani kupitia mtandao wa kijamii wa
Instagram, ambapo ameoneoakana akiibusu nembo ya The Rossoneri.
Kama hilo halikutosha, Balotelli ameandika maandishi yaliyoambatana
na picha hiyo kwa kusisitiza anaipenda sana AC Milan zaidi ya ilivyokua
siku za nyuma wakati akiwa klabuni hapo kabla ya kuuzwa huko Anfield
mwezi August mwaka 2014.
Balotelli, bado hajabahatika kujumuishwa kwenye kikosi cha kwanza cha
AC Milan katika michezo ya ligi ya nchini Italia, zaidi ya kucheza
mchezo uliowashirisha wachezaji wa akiba wakati wa mchezo dhidi ya
Empoli ambapo alibahatika kufunga bao lililoipa ushindi timu yake wa
mabao mawili kwa moja.
Hata hivyo kuna uwezekano akacheza mchezo wa mwishoni mwa juma hili ambapo AC Milan watawakabili Inter Milan kwenye uwanja wa San Siro.
0 comments:
Post a Comment