Yaliyojili hii leo kimataifa Ebana best wangu kama ilivyo kawaida leo nimekuwekea hapa habari zote tatu zinasomwa kwenu na najat omary kupitia taarifa ya habari cg fm radio saa kumi jioni.
====
Mahakama ya Juu nchini RWANDA itasikiliza
pingamizi lililowekwa na chama kikuu cha upinzani
nchini humo dhidi ya juhudi za Rais PAUL KAGAME kutaka
kugombea muhula wa tatu.
Jaji IMMACULEE NYIRINKWAYA amesema baada ya
uchunguzi wa kina, mahakama hiyo ya juu imepata kila sababu
ya kusikiliza kesi hiyo na kutupilia mbali
upinzani kutoka serikalini na kesi hiyo imepangwa
kusikilizwa tarehe 23 mwezi huu.
Chama cha Democratic Green
kinapinga mabadiliko ya aya ya 101 ya
katiba ya RWANDA ambayo
inaweka ukomo wa vipindi vya urais kuwa
viwili.
Rais KAGAME alichaguliwa kwa mara ya kwanza
mwaka 2003 na akachaguliwa
tena mwaka 2010 na kwa hiyo hawezi
kugombea tena kipindi cha tatu.
Rais wa chama hicho, Bwana FRANK
HABINEZA amesema
wamefurahishwa na uamuzi wa mahakama ya
juu wa kusikiliza kesi hiyo.
Kikosi kimoja maalum cha serikali nchini SUDAN
kimeshutumiwa kwa kutekeleza mauaji ya halaiki na ubakaji wa raia katika eneo
la DARFUR MAGHARIBI tangu mwezi Februari mwaka uliopita.
Ripoti mpya ya Shirika la kutetea haki za Binadamu
inasema kikosi hicho kijulikanacho kama Rapid Support Forces kilitekeleza kile
inachosema ni unyama na ukatili katika vijiji tofauti kwenye eneo hilo.
Walioshuhudia mashambulio hayo wameeleza jinsi vikosi
hivyo maalum vya serikali vilivyowakusanya wanavijiji, vikawapiga na kuwabaka
wanawake wengi.
Mmoja wa
waathirika alisema alishuhudia wanawake kumi na saba wakibakwa katika hospitali
moja.
Mwingine
alisema aliwaona wanawake na wasichana wakibakwa na kisha kuingizwa katika
nyumba moja iliyochomwa moto bado wakiwa ndani.
====
NA
Usafiri wa treni nchini DENMARK umejea tena baada ya kusitishwa kwenda na kutoka UJERUMANI baada
ya kutokuelewana kati ya polisi na mamia ya wahamiaji.
Kundi moja la wahamiaji lilikataa kushuka katika treni
waliyokuwemo kwa madai ya kutaka kusafiri kwenda SWEDEN ambayo ina sheria nzuri
ya uhamiaji kushinda DENMARK.
Polisi wamekuwa wakiwazuia mamia yawahamiaji waliokuwa
wakitembea kwa miguu nchini DENMARK kwa lengo la kwenda SWEDEN.
Habari zinasema baadhi ya wahamiaji wamekuwa wakiwahadaa
polisi kwa kujificha katika magari ama katika matrekta yanayokokotwa na farasi.
NAJJAT OMAR,CGFM
Bofya play kusikiliza hapa chini best....
0 comments:
Post a Comment