Mratibu wa
mradi wa PAMOJA TUWALEE katika manispaa ya TABORA amewataka baadhi ya wanaume
kuacha tabia ya kutekeleza familia zao kutokana na watoto wao kukumbwa na
tatizo la ulemevu.
Akibainisha
hayo mratibu mkuu wa mradi huo bwana DEUS SHUMBI amesema hayo nyumbani kwa bi
ZUBEDA HARUNA ambaye alikimbiwa na mumewe kutokana na mtoto wake kukumbwa na
ulemavu
Bwana shumbi
amesema kuwa hiyo siyo njia sahihi ya kutatua tatizo bali ni njia ya kuongeza
tatizo ndini ya familia.
Kwa upande
wake bi ZUBEDA HARUNA ambaye ndiye mama mzazi wa mtoto MWAMVUA JUMA amebainisha
kuwa chanzo kikubwa cha mumewe kumkimbia ni kutokana na mwanae kupata ulemavu wa
mtoto waona mpaka sasa hana uwezo wa kusimama wala kufanya kitu chochote.
Naye MWMVUA
JUMA mabaye ni mtoto mlemavu aliyetelekezwa na baba yake miaka kumi na tano
iliyopita amesema maumivu anayoyap[ata
ni tumbo lake kuumia kwa muda mrefu ,kushindwa kula chakula kama wenzake na
kuhitaji kuwa katika hali ya kawaida kama binadamu wengine.
Hata hivyo
bi ZUBEDA amewaomba wananchi na watanzania kwa ujamla kumsaidia kwa msaada wa
pesa ili aweze kufanikisha matibabu ya
mwanae kwani mpaka sas hajishughulishsi na kazi yeyote na anashindwa
kumuhudumia.
Baadhi ya
majirani wananoishi kata ya CHEMCHEM katika manispaa ya TABORA MWAJUMA SALUM
pamoja na MWANAIDI SALEHE wamesema mazingira anayoishi mtoto huyo ni magumu
kupita kiasi kwani familia haina uwezo wa kifedha .
Mtendaji wa
kata ya CHEMCHEM bwana SALUM KAMBI ametowa wito kwa wananchi na mashirika ya
kiserikali na yasiyo ya kiserikali kutoa msaada kwa mtoto huyo ili aweze kupatiwa
matibabu.
Aidha Bi
ZUBEDA amewaomba wananchi kuweza kumsaidia kwa kumchangia chochote yeye pamoja na mwanae ambaye ni mlemavu
kupitia namba za siku 0688839371 au 0752925689.
Bofya play kusikiliza hapa chini....
0 comments:
Post a Comment