728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, September 10, 2015

    Wakazi wa Manispaa ya TABORA wametakiwa kuboresha usafi wa mazingira ili kujikinga na ugonjwa hatari wa kipindupindu(AUDIO).




    Wakazi wa Manipaa ya TABORA wametakiwa kuboresha usafi wa mazingira ili kujikinga na ugonjwa hatari wa kipindupindu.


    Katika mahojiano maalumu na CGFM, Afisa Afya wa Manispaa ya TABORA,Bwana VEDASTUS CHEYO amesema baadhi ya njia za kujikinga na ugonjwa wa kipindupindu ni kuhakikisha mazingira yanakuwa katika hali ya  usafi,kujenga choo bora na kukitumia na kunawa mikono kwa maji safi na salama kwa kutumia sabuni baada ya kutoka chooni.


    Bwana CHEYO amewatahadharisha wakazi wa manispaa ya TABORA kuwa makini  na ugonjwa hatari wa kipindupindu kwa sababu unasababisha kifo kutokana na ukosefu wa maji na madini mwilini baada ya kuharisha na kutapika.


    Ameongeza kuwa ugonjwa  wa kipindupindu pia husababisha kushuka kwa uchumi katika familia kutokana na shughuli za uzalishaji mali kusimama ili kumhudumia mgonjwa na kushiriki katika misiba.


    Ugonjwa huo tayari umesababisha vifo kwa watu kadha mkoani  DAR ES SALAAM na sasa umeenea hadi mikoa ya MOROGORO na PWANI.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Wakazi wa Manispaa ya TABORA wametakiwa kuboresha usafi wa mazingira ili kujikinga na ugonjwa hatari wa kipindupindu(AUDIO). Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top