728x90 AdSpace

  • Latest News

    Sunday, September 13, 2015

    Kenya yazindua kumbukumbu kuwaenzi walioteswa katika vita ya Mau Mau.

    Kumbukumbu maalumu kwa ajili ya kuwaenzi wahanga wa mateso yaliyosababishwa wakati wa utawala wa hali ya hatari wa Uingereza wakati wa vita ya Mau Mau imezinduliwa  nchini Kenya.
     Kumbukumbu hiyo ambayo pia inaungwa mkono na Uingereza ilizinduliwa hapo jana na kushuhudiwa pia na  maelfu ya watu  wakiwemo wale walioshiriki katika vita hiyo ya Mau Mau. 
    Maelfu  ya wakenya ambao kwa sasa ni watu wazima walielezea jinsi walivyopigwa ikiwa ni pamoja na kunyanyaswa kijinsia na maafisa wa utawala wa kiingereza  wakijaribu kuzima harakati zao za ukombozi wakati makundi  kadhaa ya wakenya yalipowashambulia maafisa  na wakulima wa kiingereza waliokuwa wanashikilia maeneo makubwa ya ardhi yenye rutuba nchini humo.
     Balozi wa Uingereza nchini humo  amesema  kumbukumbu hiyo inafanyika ikiwa ni sehemu ya makubaliano yaliyofikiwa nje ya mahakama kati ya wapiganaji hao wakongwe wa vita ya Mau Mau  na serikali ya Uingereza.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Kenya yazindua kumbukumbu kuwaenzi walioteswa katika vita ya Mau Mau. Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top