728x90 AdSpace

  • Latest News

    Sunday, September 13, 2015

    MIDO NAFASI INAYOMFAA NGASSA FS APIKA MABAO MAWILI FREE STATE IKIUA 3-0 CHIPPA UTD.

    KIUNGO wa kimataifa wa Tanzania, Mrisho Khalfan Ngassa leo ametoa pasi za mabao mawili, timu yake, Free State Stars ya Afrika Kusini ikipata ushindi wa kwanza katika Ligi Kuu ya Absa baada ya kuifunga mabao 3-0 Chippa United.
    Nyota ya ngassa yaanza kung'ara sauz.
      
    Ngassa ambaye alichezeshwa nafasi ya kiungo leo, alitoa pasi ya bao la kwanza lililofungwa na Andrea Fileccia dakika ya 34 na la tatu lililofungwa na Andrea Fileccia dakika ya 84.
    Bao la tatu la Free State katika mechi hiyo kwenye Uwanja wa nyumbani, lilifungwa na Danny Venter dakika ya 77.


    Huo ni mwanzo mzuri kwa kocha mpya Mjerumani Ernst Middendorp aliyerithi mikoba ya Mmalawi Kinnah Phiri aliyejiuzulu baada ya timu kupoteza mechi tatu mfululizo za mwanzo katika Ligi Kuu ya Afrika Kusini 1-0 kutoka kwa Mpumalanga Blac Aces, 4-0 kutoka kwa Kazier Chiefs na 2-1 mbele ya Ajax Cape Town.
      Ngassa alisajiliwa Mei mwaka huu na Free State ya Bethelehem baada ya kocha Phiri kuvutiwa na soka yake akiwa anacheza Yanga SC ya Tanzania, leo alikuwa kivutio mno akicheza nafasi ya kiungo.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: MIDO NAFASI INAYOMFAA NGASSA FS APIKA MABAO MAWILI FREE STATE IKIUA 3-0 CHIPPA UTD. Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top