728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, September 15, 2015

    MBOWE: UCHAGUZI wa LUSHOTO usogezwe Mbele



    Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe ameitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi kusogeza mbele tarehe ya uchaguzi wa mbunge kwenye Jimbo la Lushoto ili kuwapa nafasi ya kujiandaa kupata mgombea mwingine mwenye sifa ya kupigania maslahi ya wananchi wa jimbo hilo kama ilivyokuwa kwa Mohamed Mtoi aliyefariki dunia kwa ajali ya gari juzi.
    Mbowe aliyasema hayo wakati akizungumza katika mazishi ya Mtoi yaliyofanyika jana kwenye Kijiji cha Mkuzi Kwekino, Lushoto mkoani Tanga na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa chama hicho akiwamo Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Salum Mwalimu na Mbunge wa Mwnyekiti wa Baraza la Wanawake, Halima Mdee.
    Mamia ya wananchi wa jimbo hilo walijitokeza kuhudhuria mazishi ya Mtoi aliyekuwa pia akigombea kwa niaba ya muungano wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) vya NCCR-Mageuzi, NLD na Chama cha Wananchi (CUF)
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: MBOWE: UCHAGUZI wa LUSHOTO usogezwe Mbele Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top