728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, September 1, 2015

    WANANCHI WATAKIWA KUMSAIDIA ILI AWEZE KUPATA MATIBABU.


    Mratibu wa mradi wa PAMOJA TUWALEE katika manispaa ya TABORA amewataka baadhi ya wanaume kuacha tabia ya kutekeleza familia zao kutokana na watoto wao kukumbwa na tatizo la ulemevu.


    Akibainisha hayo mratibu mkuu wa mradi huo bwana DEUS SHUMBI amesema hayo nyumbani kwa bi ZUBEDA HARUNA ambaye alikimbiwa na mumewe kutokana na mtoto wake kukumbwa na ulemavu

    Bwana shumbi amesema kuwa hiyo siyo njia sahihi ya kutatua tatizo bali ni njia ya kuongeza tatizo ndini ya familia.


    Kwa upande wake bi ZUBEDA HARUNA ambaye ndiye mama mzazi wa mtoto MWAMVUA JUMA amebainisha kuwa chanzo kikubwa cha mumewe kumkimbia ni kutokana na mwanae kupata ulemavu wa mtoto waona mpaka sasa hana uwezo wa kusimama wala kufanya kitu chochote.


    Naye MWMVUA JUMA mabaye ni mtoto mlemavu aliyetelekezwa na baba yake miaka kumi na tano iliyopita  amesema maumivu anayoyap[ata ni tumbo lake kuumia kwa muda mrefu ,kushindwa kula chakula kama wenzake na kuhitaji kuwa katika hali ya kawaida kama binadamu wengine.

    Hata hivyo bi ZUBEDA amewaomba wananchi na watanzania kwa ujamla kumsaidia kwa msaada wa pesa  ili aweze kufanikisha matibabu ya mwanae kwani mpaka sas hajishughulishsi na kazi yeyote na anashindwa kumuhudumia.

    Baadhi ya majirani wananoishi kata ya CHEMCHEM katika manispaa ya TABORA MWAJUMA SALUM pamoja na MWANAIDI SALEHE wamesema mazingira anayoishi mtoto huyo ni magumu kupita kiasi kwani familia haina uwezo wa kifedha .


    Mtendaji wa kata ya CHEMCHEM bwana SALUM KAMBI ametowa wito kwa wananchi na mashirika ya kiserikali na yasiyo ya kiserikali kutoa msaada kwa mtoto huyo ili aweze kupatiwa matibabu.


    Aidha Bi ZUBEDA amewaomba wananchi kuweza kumsaidia kwa kumchangia chochote  yeye pamoja na mwanae ambaye ni mlemavu kupitia namba za siku 0688839371 au 0752925689.      
    Bofya play kusikiliza hapa chini....
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: WANANCHI WATAKIWA KUMSAIDIA ILI AWEZE KUPATA MATIBABU. Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top