728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, September 10, 2015

    Haya ndiyo malalamiko ya wananchi wa TABORA manispaa kwa Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira TUWASA(AUDIO)


    wananchi wa mtaa wa KIYUNGI,kata ya KITTE katika manispaa ya TABORA wameilalamikia Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira  mjini TABORA–TUWASA- juu ya maji machafu yanayotiririka katika maeneo yao wakati Mamlaka inaposafisha matenki ya kuhifadhia maji.
     

    Wakizungumza na CGFM wananchi hao, wamesema kitendo cha maji hayo kutiririshwa  katika maeneo yao yanasababisha uharibifu wa barabara na kuhatarisha afya za watoto wanaochezea kwenye maji hayo.


     Pia wameitaka TUWASA kuboresha miundo mbinu ya kupitishia maji hayo na kuweka ulinzi wa kutosha katika maeneo yanayozunguka matenki hayo kwa ili kuepuka uharibifu wa miundombinu ya mamlaka hiyo.


    Akizungumzia malalamiko hayo, Afisa Uhusiano wa TUWASA, Bi NAJBA BATENGA amesema mamlaka haijawahi kupokea malalamiko yoyote kutoka kwa wananchi wa mtaa wa KIYUNGI kuhusu kero ya kutiririshwa kwa maji machafu katika maeneo yao.


    Hata hivyo TUWASA imesema itatoa ufafanuzi juu ya kero hiyo baada ya wiki moja. 

    BARIKI MMBAGA.

    BOFYA PLAY KUSIKILIZA HAPA CHINI....
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Haya ndiyo malalamiko ya wananchi wa TABORA manispaa kwa Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira TUWASA(AUDIO) Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top