728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, September 22, 2015

    Wanafunzi Sekondari Magoto na Manga walala sakafuni

    Wanafunzi wa kidato cha tano na sita katika shule za Sekondari Magoto na Manga zilizopo katika Wilaya Tarime mkoani Mara, wamelalamikia kitendo cha kulala sakafuni  kwa zaidi ya mwaka moja sasa huku pia wakikosa chakula na maji.

    kali ichukue hatua za haraka za kutatua tatizo hilo ili wapate huduma bora kwa lengo la kuinua kiwango chao cha elimu.

    Wakizungumza mwishoni kwa wiki kwa nyakati tofauti, baadhi ya wanafunzi ambao waliomba kutotajwa majina yao, walidai kwamba wamekuwa wakilala sakafuni kwa muda mrefu huku shule hizo zikishindwa kuwapa chakula na maji kwa ufasaha.

    “Tuna shida kubwa katika shule zetu, tulala chini kutokana na kutokuwapo kwa vitanda kwenye mabweni, pia chakula na maji ni vya shida,” alisema mmoja wa wanafunzi hao.

    Aidha, walisema baada ya kuwapo kwa hali hiyo, baadhi ya wanafunzi wenzao walijitolea kuuliza uongozi wa elimu wa wilaya, lakini walijibiwa vitanda vinatengenezwa.

    Hata hivyo, walisema mpaka sasa zaidi ya mwaka mmoja unamalizika hakuna vitanda.

    Baadhi ya wazazi wa wanafunzi wanaosoma katika shule hizo walidai kushangazwa na hali hiyo licha ya kutoa michango inayotakiwa na uongozi wa shule hizo.

    “Mara kwa mara watoto wetu wanatupigia simu kutuambia hali ilivyo, pia wanalalamikia kutopata chakula na maji, jambo linalowafanya wasome kwa shida,” alisema mmoja wa wazazi hao, John Joseph, kwa niaba ya wenzake.

    Ofisa Elimu Sekondari wa Wilaya ya Tarime, hakupatikana kuzungumzia malalamiko hayo ya wanafunzi na wazazi.
    Hata hivyo, Mkuu wa Shule ya Sekondari Magoto, Anthony Charles, alithibitisha kuwapo kwa tatizo la vitanda na chakula shuleni hapo.

    Charles alisema walitoa zabuni ya utengenezaji wa vitanda hivyo lakini mpaka sasa havijakamilika.
    CHANZO: NIPASHE.

    CHANZO: NIPASHE
    - See more at: http://edwinmoshi.blogspot.com/2015/09/wanafunzi-sekondari-magoto-na-manga.html#sthash.8YPULf4g.dpuf
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Wanafunzi Sekondari Magoto na Manga walala sakafuni Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top