728x90 AdSpace

  • Latest News

    Sunday, September 13, 2015

    Mfalme wa Saudia aapa kuchunguza chanzo cha ajali.


    Mfalme Salman wa Saudi Arabia ameapa kuwa atafanya kila awezalo kugundua kilichosababisha ajali ya winchi iliyouwa watu 107 katika Msikiti Mtukufu wa Makka hapo juzi. Akitembelea msikiti huo hapo jana, Mfalme Salman alisema matokeo ya uchunguzi huo yatawekwa hadharani kwa umma. Winchi ya ujenzi ilianguka siku ya Ijumaa kufuatia upepo mkali kwenye mji huo ambao unatambuliwa kuwa eneo takatifu kwa waumini wa Kiislamu. Ajali hii imetokea wakati mamilioni ya Waislamu kutoka kote ulimwenguni tayari wameanza kuwasili mjini Makka kwa ajili ya ibada ya kila mwaka ya Hijja. Miongoni mwa waliopoteza maisha ni raia wa India na Indonesia. Mfalme Salman aliwatembelea pia majeruhi waliolazwa hospitalini, wakiwemo kutokea Iran, Uturuki, Misri na Pakistan.
    DW IDHAA YA KISWAHILI.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Mfalme wa Saudia aapa kuchunguza chanzo cha ajali. Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top