728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday, September 7, 2015

    Mwanafunzi mwerevu apata alama 0 !


    Maelfu ya wazazi na wanafunzi wamejitokeza kumuunga mkono mwanafunzi mmoja shupavu aliyepata sufuri katika mtihani wake wote wa mwisho.
    Amini usiamini,Mariam Malaka ambaye amekuwa mwanafunzi wa kupigiwa mfano nchini Misri kutokana na alama za juu alizopata katika mitihani ya awali, alikuwa na matarajio ya kuzoa alama ya juu zaidi yaani A itakayomwezesha kujiunga na chuo cha mafunzo ya daktari lakini wapi ?
    Katika mtihani wake wa mwisho Mariam Malak alipewa alama za chini zaidi .
    Hii ikimaanisha kuwa, bi Malak hakuandika hata herufi moja aliyojibu kikamilifu.
    Bi Mariam Malak anashuku kuwa kulitokea kosa kubwa kwani yeye alivyofanya mtihani huo hadhani kama angeufeli.
    ''Kwa kweli sikuamini macho yangu eti nimefeli mtihani wa mwisho'' bi Mariam Malak aliiambia BBC
     
    Alizimia alipotafuta jina lake na akaikosa katika orodha ya watahiniwa waliopasi mtihani wao wa mwisho.
    Malak alikuwa hajaufeli mtihani mmoja bali alikuwa amezoa sufuri katika masomo yote saba.
    Yaani alikuwa ameambulia sufuri juu ya mia 0% katika masomo yote saba.
    ''Hii sio kweli''
    Familia yake inadai kuwa huwenda malak ameangushwa mtihani wake wa mwisho maksudi tu kwa sababu ya hila.
    Awali ilidhaniwa kuwa alichukiwa kwa sababu yeye ni wa kutoka kwenye tabaka la Wamisri wachache ambao ni wakristo wa kicoptic lakini dhana hio ilikataliwa.
    Familia yake inahofia huenda hii ikawa ni njama ya kumpokonya mwanawao ndoto yake ya kuwa daktari
     
    Wizara ya Elimu imelazimika kumpa mtihani wa kubaini iwapo hati iliyowakilishwa kwa jina lake ni yake haswa ama ni ghushi, hata hivyo ikatoa uamuzi kuwa ilikuwa yake haswa.Hata hivyo maelfu ya watu waliotazama nakala za hati aliyoandika kwenye runinga walisema hazifanani kabisa na zile zilizopewa jina lake.
    Kufuatia tofauti hiyo, ukurasa ulianzishwa kwa nia ya kuishinikiza wizara ya elimu kuingilia kati kutanzua kitendawaili hicho.
    Ukurasa huo unawafuasi takriban 30,000 kufikia sasa.
    Tayari watu kadha wamejitokeza kugharamia malipo yake yote ya chuo kikuu.
    Ndugu yake Mina anasema kuwa wanashuku majibu yake yalipewa mtu mwengine.
        BBC.
     
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Mwanafunzi mwerevu apata alama 0 ! Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top