728x90 AdSpace

  • Latest News

    Sunday, September 13, 2015

    Thiago aurefusha mkataba wake na Bayern.

    Kiungo wa Bayern Munich Thiago Alcantara amekubali kuurefusha mkataba wake na klabu hiyo kwa miaka miwili hadi 2019. Mhispania huyo analenga kujaza pengp la Bastian Schweinsteiger. 

    Kwa mujibu wa gazeti la Ujerumani la “Bild” Thiago sasa ataweka mfukoni kiasi cha hadi euro milioni tisa kwa mwaka katika marupurupu.
    Mwenyekiti wa Bayern Karl-Heinz Rummenige amesema wana furaha kwa Thiago amekubali kubakia katika klabu hiyo.
    Mhispania huyo hajawa na mwanzo mzuri katika klabu yake hiyo tangu alipojiunga mwaka wa 2013 kutoka Barcelona kutokana na matatizo ya goti. Alikuwa mkekani kwa karibu mwaka mmoja. Alirejea Aprili 2015 na kufikia sasa amecheza michuano 25 ya Bundesliga huku akifunga magoli manne na kusaidia katika mengine manne.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Thiago aurefusha mkataba wake na Bayern. Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top