728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, February 12, 2016

    Tamasha la ‘Sauti za Busara’ Zanzibar, halitafanyika mwaka 2016, sababu zipo hapa.

    Waandaaji wa Tamasha kubwa la muziki wa ‘live’ la Sauti za Busara linalofanyika kila mwaka Zanzibar, wametangaza kutokufanyika kwa tamasha hilo mwaka huu kwa ukosefu wa udhamini.

    Akizungumza na mwandishi wa mtandao huu mmoja wa waandaji hao Journey Ramadhan, amesema wamekosa wadhamini wa kutoa fedha kwa ajili ya uendeshaji wa Tamasha hilo.

    “Tunaweza kusema ni ukosefu wa udhamini ambao unasababisha tamasha kutokufanyika mwaka huu, na hali hii ya ikiendelea inawezekana hata 2017 lisifanyike pia” Alisema.

    Bwana Ramadhan amewaomba wadau na wapenda sanaa nchini, kujitokeza kudhamini Tamasha hilo, kwani faida zitokanazo na tamasha hilo ni kubwa kwa Tanzania.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Tamasha la ‘Sauti za Busara’ Zanzibar, halitafanyika mwaka 2016, sababu zipo hapa. Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top