728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, February 4, 2016

    Leo ni siku ya ‘Saratani’ duniani, Serikali ina haya machache.

    Katibu Mkuu wa WIZARA ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto , Dk. Ulisubisya Mpoki amesema kuwa Saratani ni ugonjwa ambao unaathiri watu wa rika na jinsia zote; watoto, watu wazima, wake kwa waume.

     Takwimu za Shirika la Kimataifa la Atomiki la Utafiti wa Saratani (IARC) na Shirika la Afya Duniani (WHO) zinaelezea kwamba kila mwaka duniani kunatokea wagonjwa wapya wa saratani wanaokadiriwa kufikia milioni 14.1, kati ya hao, zaidi ya wagonjwa milioni 8.2 hufariki dunia kutokana na ugonjwa wa Saratani, hii husababishwa kwa wagonjwa kuchelewa kufikishwa kwenye vituo vya kutolea huduma za afya. Vifo vya ugonjwa wa Saratani ni asilimia 13 ya vifo vyote vinavyotokea duniani (WHO). 

    Tizama video hapa chini kwenye kongamano la Saratani;



    Amesema tatizo la Saratani limekuwa likiongezeka na kukua, kila mwaka, Takribani wagonjwa wapya wapatao 44,000 hugundulika na saratani za aina mbalimbali nchini, hii ni sawa asilimia 10 tu (4,400) kati ya wagonjwa wote wanaofanikiwa kufika katika Taasisi ya Saratani Ocean Road ili kuweza kupata tiba.


    Kati ya hao wanaobahatika kufika katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (takribani asilimia 80) hufika wakiwa katika hatua za mwisho za ugonjwa (Hatua ya 3 na ya 4), hali ambayo hupunguza uwezekano wa wagonjwa kuweza kupona maradhi hayo.

    Dk.Mpoki kwa mujibu wa taarifa kutoka Taasisi ya Saratani ya Ocean Road hapa nchini zinaonyesha kwamba aina za Saratani zinaoongoza ni kama ifuatavyo:

    Kwa upande wa wanaume,Saratani ya Ngozi ,Saratani ya Koo, Saratani ya Tezi Dume, pamoja na Saratani ya Tezi,na wanawake ni Saratani ya Shingo ya Kizazi, Saratani ya Ngozi, Saratani ya Matiti, pamoja na Saratani ya Koo.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Leo ni siku ya ‘Saratani’ duniani, Serikali ina haya machache. Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top