728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, February 5, 2016

    Monalisa: Nilishawahi ‘kulizwa’ baada ya kumuachia mtu anisambazie ‘Filamu’ yangu.

    Muigizaji Grade one Tanzania,Vyone ‘Monalisa’Cherry, amewataka wasanii wenzie Batuli na Ray kumaliza tofauti zao kwa amani bila kufikishana mbele ya vyombo vya Sheria.


    Huku akifichua changamoto ya kutapeliwa aliyowahi kufanyiwa katika usambazaji wa filamu yake. “Ray na Batuli wote nyie ni ndugu, hakuna haja ya kujibizana kwenye mitandao au kupelekana kwenye sheria malizeni tu”

    Monalisa amesema aliwahi kumpa mtu (hakupenda kumtaja jina) filamu yake amsambazie, lakini aliishia ‘kulizwa’ baada ya msambazaji huyo kuingia mitini.
     
    “Nilimpa anisaidie kusambaza lakini mpaka leo hela sijaiona na nikimpigia simu anadai ana vikao mara yuko busy mpaka nikakata tamaa afu si tunafanya kazi kiujamaa na kindugu muda mwingine” Alisema
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Monalisa: Nilishawahi ‘kulizwa’ baada ya kumuachia mtu anisambazie ‘Filamu’ yangu. Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top