728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, February 6, 2016

    Neville kusononeshwa baada ya Valenci kuadhibiwa na Barcelona.

    Klabu ya Valencia chini ya nyota wa zamani wa Manchester United,Gary Neville ilipokea kichapo cha mwaka kutoka kwa Barcelona katika nusu fainali ya michuano ya Copa Del Rey Baada ya kubebeshwa magoli saba.

    Mechi hiyo ya mkondo wa kwanza ilichezewa uwanja wa Nou Camp.
    Luis Suarez alifunga mabao manne,huku nyota wa Argentina Lionel Messi naye akijizolea magoli matatu.

    Valencia walidhofishwa zaidi na hatua ya beki Shkodran Mustafi kumchezea visivyo Messi kipindi cha kwanza,kosa lililomfanya kufukuzwa uwanjani. 

    Neville hajashinda mechi hata moja ligini kati ya nane alizosimamia tangu kuchukua usukani Desemba,mwaka jana.

    Neville alikuwa amerejea uwanja ambao enzi yake ya uchezaji alipata ushindi mkubwa na muhimu sana.

    Akiwa na umri wa miaka 24,alikuwa kwenye timu ya United iliyoshinda Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya baada ya kujikwamua dhidi ya Bayern Munich fainali ya 1999 uwanjani Nou Camp.

    Akizungumza baada ya mechi hiyo dhidi ya Barca,Neville alisema siku hiyo ni moja ya siku zenye machungu zaidi katika maisha yake katika ulimwengu wa soka.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Neville kusononeshwa baada ya Valenci kuadhibiwa na Barcelona. Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top