728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, February 17, 2016

    RONALDO AKIMBIA MKUTANO NA WAANDISHI BAADA YA KUULIZWA SWALI HILI;

    CRISTIANO Ronaldo amejikuta akikimbia mkutano na waandishi wa habari na kumuacha kocha wake Zinedine Zidane akiendelea na mkutano huo.

    Ronaldo aliulizwa kwamba urafiki na ukaribu uliopo kati ya Messi, Neymar na Suarez ndiyo unaochangia wachezaji hao kufunga goli nyingi?   
     
    "Nilipokuwa Manchester nilikuwa nikikutana na Paul Scholes, Rio Ferdinand  na Ryan Giggs tulikuwa tukiambiana usiku mwema na za asubuhi na tulikuwa hatari mno,"

    Cristiano aliendelea kuwaambia umoja bila kazi uwanjani ni bure huku akionekana kukerwa na swali aliloulizwa kuwa anachukuliaje kucheza mechi nne ugenini pasipo kufunga bao lolote.

    Ronaldo aliwajibu kuwa "Kama unaweza nitajie mchezaji aliyefunga magoli mengi zaidi yangu mimi ugenini ?, Hakuna " 

    Ronaldo aliondoka kwenye mkutano huo huku akimwacha kocha wake akiendelea.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: RONALDO AKIMBIA MKUTANO NA WAANDISHI BAADA YA KUULIZWA SWALI HILI; Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top