728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, February 26, 2016

    BAADA YA BLATTER KUTAWALA KWA MIAKA 18 HUYU NDIYE BOSI MPYA WA FIFA.

    HATIMAYE Gianni Infantino ameshinda kiti cha urais wa FIFA baada ya kupata kura 115 dhidi ya 88 za mpinzani wake Sheikh Salman bin Ebrahim al-Khalifa  
    Upigaji kura wa kuamua atakayekuwa rais wa shirikisho la soka duniani FIFA uliingia raundi ya pili baada ya kukosekana kwa mshindi wa moja kwa moja kwenye raundi ya kwanza. Mshindi alitakiwa kupata theluthi mbili ya kura zote.
    Aliyekuwa katibu mkuu wa UEFA,  Gianni alipata kura 88, ikiwa ni kura tatu zaidi ya mpinzani wake wa karibu Sheikh Salman hivyo kuamriwa uchaguzi uingie katika hatua ya pili kwa mara ya kwanza tangu ilipotokea hivyo mwaka 1974.
    Wajumbe kutoka mataifa 207 yanayotambuliwa na Fifa duniani wameshiriki uchaguzi huo mjini Zurich kuamua mrithi wa Sepp Blatter.
    Kabla ya upigaji kura kuanza, mageuzi kadha yalipitishwa, lengo likiwa kufanya Fifa kuwa na uwazi na uwajibikaji zaidi.
    Kufuatia mabadiliko hayo, mishahara yote ya maafisa wa Fifa inafaa kuwekwa wazi siku za usoni.Kutakuwa pia na kipimo kwenye muhula wa urais.
    Baraza jipya pia litaundwa kuchukua nafasi ya kamati kuu tendaji, ambalo litakuwa na mwakilishi mwanamke kutoka kila shirikisho.
    chanzo BBC.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: BAADA YA BLATTER KUTAWALA KWA MIAKA 18 HUYU NDIYE BOSI MPYA WA FIFA. Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top