728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, February 12, 2016

    WASIRA: SINA HAKIKA KAMA MAGUFULI ANABANA MATUMIZI.

    Mwanasiasa mkongwe aliyekuwa waziri kwenye Serikali za Awamu Nne za Kwanza, Stephen Wasira amesema hana uhakika kama muundo wa Serikali ya Rais John Magufuli unapunguza matumizi ya fedha za umma.


    Wasira anakuwa waziri wa tatu wa Serikali ya Awamu ya Nne kuzungumzia sera za kubana matumizi za Rais Magufuli, baada ya Bernard Membe na Dk Makongoro Mahanga kusema kuunganisha wizara na kubakia na idadi kubwa ya makatibu wakuu si kubana matumizi.

    Baraza ambalo Rais Magufuli alilitangaza lina mawaziri 34, ikiwa ni pungufu ya mawaziri 20 ikilinganishwa na baraza la mwisho la Rais Jakaya Kikwete, huku kukiwa na wizara 18, baadhi zikiwa zimebakia na makatibu wake wakuu licha ya kuunganishwa.
    Akizungumza kwenye mahojiano maalumu na Mwananchi, Wasira alisema licha ya Rais Magufuli kupunguza idadi ya mawaziri ikilinganishwa na mtangulizi wake, jambo hilo halimaanishi kwamba Serikali itatumia fedha kidogo.

    Wasira, ambaye alikuwa miongoni mwa wana-CCM waliojitokeza kutaka kuteuliwa na chama hicho kuwania urais, alisema mtazamo kuhusu baraza la mawaziri unategemea malengo ya kiongozi husika.
    ========================================================

    TANGAZA NASI KWA VITU VIFUATAVYO;
    1. Biashara / Maduka na Bidhaa / Ofisi 2. Kuuza Nyumba / Kupangisha 3. Kuuza Magari / Pikipiki 4. Kuuza Viwanja / Mashamba 5. Matangazo Mbalimbali 6. Matangazo ya Mikutano / Sherehe 7. Matangazo Shule / Course za Masomo Mbalimbali 8. Hotel / Restaurat

    Tunapokea matangazo  yako sasa Tangaza na TBN_MUSSANKONINGO.BLOGSPOT.COM  kukuza Bishara yako.. Wasiliana nasi Kwa simu namba 0755933877/0787260182.   Au EMAIL@MUSSABAKARINKONINGO@GMAIL.COM.




     
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: WASIRA: SINA HAKIKA KAMA MAGUFULI ANABANA MATUMIZI. Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top